GOOGLE YAZINDUA SIMU YA KISASA AFRICA - HOT 2
Google imezindua simu ya kisasa ya bei rahisi barani Afrika. Simu hiyo,
Hot 2 ambayo haina 'makorokoro' mengi itaanza kupatikana katika nchi
sita za Afrika. Itagharimu kati ya dola 85 na 100. Licha ya kuwa si watu
wengi watakuwa na uwezo wa kuinunua, lakini ni bei rahisi kulinganisha
na iPhone ambayo inauzwa hadi dola 1,000. Uzinduzi huu ni juhudi za
Google kujaribu kulikamata soko linalokua kwa kasi la simu za kisasa,
ambapo watumiaji wengi bado hawana uwezo wa kuwa na vifaa vinavyoweza
kuuganishwa kwenye mtandao wa internet.
Dunia hii tutaona kila aina yA simu..., yetu macho!
ReplyDelete