SHAMBA LA BIBI

SHAMBA LA BIBI

Thursday, 20 August 2015

SIRI IMEFICHUKA! CCM YAIMALIZA UKAWA CHINICHINI!..SHUHUDIA WALICHOFANYA SASA HAPA


WAKATI vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) ukiwa bize kumtambulisha mgombea wake wa urais, Edward Lowassa kwa mbwembwe mikoani, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinadaiwa kujipanga kimyakimya huku kikitekeleza mikakati yake chinichini, Risasi Mchanganyiko limeambiwa.

Mmoja wa maofisa wa chama hicho kutoka ofisi ndogo, Lumumba jijini Dar es Salaam, amesema hawatishiki na ‘amshaamsha’ inayoendelea mikoani katika kumnadi mgombea huyo wa Ukawa, kwani wanajua kitu gani wanapaswa kufanya ili kujipatia ushindi kwenye uchaguzi mkuu ujao.
“Wala usiwe na hofu kaka, kama wao wanajua hii, sisi tunajua huu, unafikiri wao wana akili kuliko sisi? Usije ukadhani tumelala tunawashangaa, sisi tupo bize sana katika mikakati yetu, ingawa tunafanya kimyakimya, waache wajisahau watashtukia tunaibuka na ushindi wa kishindo kama kawaida,” alisema ofisa huyo, aliyeomba hifadhi ya jina lake.

Alisema kinachofanywa na Ukawa hivi sasa ni sawa na maigizo, kwani umati wa watu wanaojitokeza kwenye mikutano yao, haimaanishi kuwa ni wapiga kura, kwani wengi wao ni mashabiki ambao hata kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura, hawajajiandikisha.

Mgombea urais wa Ukawa, Edward Lowassa amekuwa akitambulishwa katika mikoa mbalimbali nchini na kujaza umati wa watu wanaojitokeza kusikiliza hotuba zake, kitu ambacho awali, kilidhaniwa kuwa kitu kinachowatisha CCM, ambao ndiyo chama dola kwa sasa.


Nipe maoni yako mdau...!

No comments:

Post a Comment