ZIJUE TOFAUTI KATI YA CHETI CHA KUZALIWA NA KITAMBULISHO CHA TAIFA
Cheti cha kuzaliwa ni nyaraka ya kwanza kabisa kwa mtu pindi tu
anapozaliwa. Kitambulisho cha Utaifa inatolewa kwa mtu aliyefikisha
miaka 18, na kiambatisho cha lazima cha kwanza ni cheti cha kuzaliwa.
- Cheti cha kuzaliwa kinaonyesha majina ya baba, mama, ulizaliwa lini
na wapi n.k papo hapo. Kitambulisho cha Taifa ni kama kadi ya bank
ilivyo matumizi ni rahisi kubeba na taarifa zingine zinazokuhusu mpaka uende ofisini katika mitambo maalum kujua taarifa zako za wapi ulizaliwa, majina ya mama, pasipoti namba (kama unayo).
- Hizi ni mamlaka mbili tofauti na sheria zinasema ni lazima kujisajili
kupata cheti cha kuzaliwa na unapofikia miaka 18 ni lazima ujiandikishe
kupata kitambulisho hicho. Nakutakia jioni njema!!
-Cheti cha kuzaliwa ni kiambatanisho muhimu kitakachokuwezesha kupata hati yako ya kusafiria (passport).
No comments:
Post a Comment