Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limepiga marufuku
wagombea urais kufanya vitendo vinavyoweza kuhatarisha usalama wa
wananchi.
Akiongea leo Jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Kanda
hiyo Suleiman Kova ametolea mfano kitendo cha jana cha mgombea urais wa
Chadema Mhe. Edward Lowassa cha kufanya ziara ya kushtukiza kwa wananchi
na kupanda daladala.
Amesema
ziara hiyo ya Mhe. Lowassa na mgombea mwenza wake Juma Duni Haji
walitembelea Gogo la Mboto, ingeweza kuhatarisha usalama wa wananchi kwa
kuwa watu wengi walikusanyika na wengine kuacha kazi zao.
No comments:
Post a Comment