Mshambuliaji wa Liverpool Mario Balotelli, 25, atakataa kujiunga na
Lazio au Sampdoria kwa mkopo kwa sababu atalipwa fedha nyingi tu za
'uzalendo' kama bado atakuwepo Anfield dirisha la uhamisho likifungwa
(Daily Mirror), Juventus wanafikiria kumchukua kiungo wa Liverpool
Lucas, 28, ambaye hakutajwa kwenye kikosi cha Brendan Rodgers dhidi ya
Stoke wiki iliyopita (Daily Express), matumaini ya Manchester United
kumsajili beki wa Real Madrid Sergio
Ramos, 29, yamekwisha baada ya beki huyo kujiandaa kuongeza mkataba wake
wiki ijayo (Guardian),meneja wa Manchester United Louis van Gaal
amesema ana matumaini kuwa mshambuliaji Wayne Rooney, 29, ataweza
kupachika mabao zaidi ya 20 msimu huu (Independent), mshambuliaji wa
Tottenham, Roberto Soldado, 30, amesafiki kwenda Spain kukamilisha
uhamisho wake kwenda Villareal (Guardian), Emmanuel Adebayos, 31, wa
Tottenham na Javier Hernandez wa Manchester United, 27, ni kati ya
washambuliaji wanaonyatiwa na West Ham (London Evening Standard),
Everton wanamtaka beki wa zamani wa kushoto wa Manchester United
Alexander Buttner, 26, kuziba nafasi ya Leighton Baines aliyeumia (Daily
Mail), Fifa imemshutumu meneja wa Chelsea Jose Mourinho kwa jinsi
alivyofarakana na daktari wa timu Dr Eva Carneiro (Daily Telegraph),
Sunderland wamekuwa na mazungumzo ya kumsajili tena mshambuliaji Fabio
Borini kwa mkopo, mwaka mmoja baada ya mchezaji huyo kukataa kwenda
Stadium of Light (Sunderland Echo), QPR wanakaribia kumsajili beki wa
Bolton Tim Ream, 27 (NBC Sports). Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa.
Share hizi na wapenda soka wote. Cheers!!
No comments:
Post a Comment