KIJANA TAJIRI AFRIKA ANATOKA TANZANIA, JE UNAMJUA NI NANI...!?!?!?
Mfanyabiashara maarufu nchini na Mbunge wa Singida Mjini (CCM), Mohammed
Dewji (pichani) kwa mara ya kwanza ameingia kwenye orodha ya mabilionea
29, akiwa tajiri kijana kuliko wote barani Afrika.
Jarida la Forbes la Marekani limemtaja Dewji (39), katika nafasi ya 24
ya matajiri wa Afrika akiwa na utajiri wa Dola 1.3 bilioni za Marekani
(Sh2.34 trilioni) unaotokana na biashara mbalimbali anazozifanya kupitia
kampuni yake ya Mohammed Enterprises (Metl Group).“Dewji alibadilisha
biashara aliyoanzisha baba yake kutoka uuzaji bidhaa na kuwa na viwanda
vya Metl,” inasema sehemu ya habari inayomuhusu bilionea huyo Mtanzania .
“Alinunua viwanda vya nguo na mafuta vilivyokuwa vinamilikiwa na
Serikali kwa bei ndogo na kuvifanya viwe na faida zaidi kwa kutumia
mtindo wa kisasa wa menejimenti,” inaongeza ripoti hiyo.
Metl ina
viwanda vya kutengeneza nguo na bidhaa nyingine za matumizi ya binadamu
vikiwamo vyakula, sabuni na vinywaji. Pia ina mapato yanayozidi Dola 1.4
milioni za Marekani (Sh2.5 trilioni) kwa mwaka.
Katika kampuni
hiyo, ambayo imekuwa na ushindani dhidi ya kampuni kubwa nyingine kama
Said Salim Bakhresa, Dewji anamiliki asilimia 75 ya hisa zote.
Kwa
mujibu wa tovuti yake, Metl inaendesha shughuli za uagizaji na
usafirishaji bidhaa kutoka na kwenda nje, uzalishaji unaohusisha nguo,
vinywaji na vyakula, usagaji nafaka, nishati na petroli na utengenezaji
baiskeli.
Pia inahusika na huduma za simu, fedha, kilimo na pia ina kitengo cha kontena kwenye Bandari ya Dar es Salaam.Dewji
anashika nafasi mbili juu zaidi ya kada maarufu wa CCM na aliyekuwa
mbunge wa Jimbo la Igunga, Aziz Rostam (50) aliyewekwa nafasi ya mwisho.Rostam
amefungana nafasi ya 26 na mabilionea wa Nigeria, Abdulsamad Rabiu na
Femi Otedola wenye utajiri wa Sh1.8 trilioni kila mmoja.Orodha
hiyo ya 29 bora inaoongozwa na bilionea wa Nigeria, Aliko Dangote akiwa
na utajiri wa Dola 15.7 bilioni za Marekani (Sh28.2 trilioni), kiwango
ambacho ni mara moja na nusu ya bajeti ya Serikali ya Tanzania ya mwaka
2014/15.
Forbes linamtaja Rostam kuwa na utajiri wenye thamani ya Dola 1 bilioni
za Marekani (Sh1.8 trilioni), kiwango ambacho kimebaki pasi na
mabadiliko kutoka orodha ya mwaka jana.
Rostam anamiliki asilimia 35 ya
hisa katika kampuni ya huduma za simu za mkononi ya Vodacom.
No comments:
Post a Comment