Keisha ni mmoja wa wasanii walioshindwa kupitia kwenye kura za
kuwapata wabunge wa viti maalum kupitia CCM lakini amesema hajakata
tamaa.
Keisha ameiambia Bongo5 kuwa ingawa alishinda katika kura za maoni, katika kura za taifa aliibuka katika nafasi ya nne.
“Zile za kwanza zilikuwa ni kura za maoni nilishinda, then kulikuwa
na kura za kitaifa ambapo nilikuwa mtu wa 4 katika watu 18,” alisema.
“Watu wanaotakiwa ni wawili, kwahiyo wawili ndio
walioshida katika upande wa walemavu. Basi maisha yanaendelea na
tunaendelea na kampeni kwa sababu ni chama changu. Lakini hii hatua
niliyofikia imenijenga kwa sababu wakati nashiriki, sikutengemea ushindi
peke yake, nilijua pia kuna kushindwa kwa sababu kuna watu walianza
hiyo safari muda mrefu. Kama hao walioshinda wawili walianzia mwaka
2010, kwahiyo mtu asiyekubali kushindwa siyo mshindani.”
No comments:
Post a Comment