
UAMUZI wa umoja wa vyama vinne vya upinzani nchini (UKAWA) wa kuachiana majimbo, umezua balaa mkoani Mtwara. Hali hiyo imetokana na uongozi wa Chama cha National League for Democracy (NLD), kudai uongozi wa Ukawa kuanzia wilayani hadi taifa umejawa na viongozi wabinafsi na wenye mizengwe.
Mwenyekiti wa NLD Mkoa wa Mtwara, Ahmed Nannyoho, alisema jana kuwa Ukawa ndani ya NLD hauna manufaa yoyote na wamejipanga kuhakikisha wanapata ushindi wa kishindo bila hata kuwa ndani ya Ukawa.
Amesema kuwa Mwenyekiti wao wa Taifa, Dk Emmanuel Makaidi, analitambua hilo licha ya kuendelea kushiriki katika mikutano ya Ukawa. Alitoa kauli hiyo wilayani Masasi jana, alipozungumza na vyombo vya habari baada ya kutakiwa kutoa ufafanuzi kuhusu idadi ya wagombea waliojitokeza kugombea ndani ya NLD mkoani Mtwara.
Ukawa unaundwa na vyama vya NLD, NCCR-Mageuzi, CUF na Chadema, na kwa mujibu wa makubaliano ya wakuu wa vyama hivyo, wataachiana majimbo katika mikoa mbalimbali nchini.
Mwenyekiti huyo wa NLD Mtwara alisema chama hicho kinatangaza rasmi kuwa hakiko tayari kuendelea na Ukawa, kwa madai kuwa umoja huo kuanzia Wilaya ya Masasi hadi ngazi ya Taifa, umejawa na viongozi wenye mizengwe na wenye ubinafsi, badala ya kujenga hoja za kuwatetea wananchi.
Kwa kusoma habari hii zaidi
Bonyeza hapa :
No comments:
Post a Comment