Jeshi
la Polisi Mkoa wa Mbeya limepiga marufuku maandamano wakati wa kumpokea
Mgombea urais wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kupitia tiketi ya
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mh. Edward Lowassa, hii leo.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi
(ACP) Ahmed Msangi ametoa agizo hilo kwa wananchi kutofanya maandamano
yoyote yawe ya miguu au pikipiki na kusema kuwa kibali chao ni mkutano
wa hadhara utakaofanyika katika viwanja vya Ruanda Nzovwe kinyume na
hapo polisi itachukua hatua kali za kisheria.
No comments:
Post a Comment