SHAMBA LA BIBI

SHAMBA LA BIBI

Thursday, 20 August 2015

GOOGLE YAZINDUA SIMU YA KISASA AFRICA - HOT 2


Google imezindua simu ya kisasa ya bei rahisi barani Afrika. Simu hiyo, Hot 2 ambayo haina 'makorokoro' mengi itaanza kupatikana katika nchi sita za Afrika. Itagharimu kati ya dola 85 na 100. Licha ya kuwa si watu wengi watakuwa na uwezo wa kuinunua, lakini ni bei rahisi kulinganisha na iPhone ambayo inauzwa hadi dola 1,000. Uzinduzi huu ni juhudi za Google kujaribu kulikamata soko linalokua kwa kasi la simu za kisasa, ambapo watumiaji wengi bado hawana uwezo wa kuwa na vifaa vinavyoweza kuuganishwa kwenye mtandao wa internet.

1 comment:

  1. Dunia hii tutaona kila aina yA simu..., yetu macho!

    ReplyDelete