CHELSEA WAIPIKU MAN UTD KUMNASA PEDRO
Chelsea wamefikia makubaliano na Barcelona kumsajili winga Pedro kwa
pauni milioni 21. Mchezaji huyo, 28, ambaye alikuwa akisakwa na
Manchester United, anasafiri kwenda London kukamilisha uhamisho wake.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Spain, amepachika mabao 99 katika mechi
326 tangu alipoanza kucheza mwaka 2008. Atakuwa mchezaji wa pili
kusajiliwa na Chelsea ndani ya wiki moja, kufuatia kuwasili kwa beki wa
kimataifa wa Ghana Abdul Baba Rahman.
No comments:
Post a Comment