![]() |
Edwad Lowassa katikati akiwa na baadhi ya viongozi wa juu wa CHADEMMA |
WAKATI wafuasi
wa vyama vya upinzani vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi ( Ukawa)
wakiwa na shangwe kutokana na kumpata Waziri Mkuu wa zamani, Edward
Lowassa kama mgombea wake wa urais katika uchaguzi mkuu wa Oktoba, ugumu
wa kiongozi huyo kuingia ikulu umebainishwa.
aliyekuwa waziri mkuu wa kwanza wa serikali ya awamu ya nne chini ya Rais Jakaya Kikwete, alijiunga na Chadema mwishoni mwa Julai mwaka huu baada ya jina lake kukatwa wakati wa mchakato wa kutafuta mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), nafasi ambayo ilitua kwa Dk. John Pombe Magufuli.
![]() |
Lowassa na mgombea mwenza Juma Duni Hajii. |
Ugumu wa kwanza unaotajwa, ni uwezekano
wa kutopigiwa kura na wafuasi wote wa Chadema, ambao kuingia kwa kada
huyo wa zamani wa CCM, kuliwagawa, kwani wapo waliokubali kwa roho moja
ujio wake na wengine ambao hawakupendezwa kabisa na jambo hilo. Mgawanyo
huo, unapunguza kura ambazo angeweza kuzipata endapo wanachama hao
wangekuwa kitu kimoja kama awali.
Ingawa aliripotiwa kuwa na wafuasi wengi
akiwa CCM, ushahidi unaonesha kuwa siyo mashabiki wake wote
wamefurahishwa na hatua yake ya kuhamia upinzani, hivyo idadi kubwa ya
wapiga kura aliokuwa akiwategemea, wameamua kuachana naye na wao
kuendelea kubakia chama tawala.
![]() |
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa na Mgombea urais kwa tiketi ya Chadema. |
Ugumu mwingine, unatokana na ukweli kuwa
licha ya Chadema kujizatiti hadi vijijini, lakini haina mtandao mpana
kama ilivyo kwa CCM, hivyo hata ile ‘amsha amsha’ inayoonekana mijini
hivi sasa, haiko vijijini, ambako chama tawala bado kina mizizi na kina
wapiga kura wengi maeneo hayo.
Jambo lingine linalotajwa kuwa ni gumu
kwa Lowassa kuingia ikulu, ni ukweli kuwa kujiweka kando kwa viongozi
wawili waliokuwa na mashabiki wengi, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk.
Wilbroad Slaa na Mwenyekiti wa Cuf, Profesa Ibrahim Lipumba
kumewachanganya mno wafuasi wao na hivyo kuwa njia panda.
Ukimya wa Dk. Slaa, anayeaminika kufanya
kazi kubwa ya kuwashawishi watu kuipenda Chadema, umewafanya baadhi ya
wafuasi wake kutokuwa na mwelekeo, hivyo kuweka uwezekano mkubwa wa watu
hao ama kupiga kura kwa wagombea wa vyama vingine au wasipige kabisa,
kitu kitakachopunguza kwa kiwango kikubwa idadi ya kura za Lowassa
kuelekea ikulu.
No comments:
Post a Comment