![]() |
Rais wa TFF, Jamal Malinzi |
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), jana lilisaini mkataba mpya na Kampuni ya simu ya Vodacom wa kudhamini Ligi Kuu Tanzania Bara wenye thamani ya Sh bilioni 6.6 kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo.
Hafla hiyo ilifanyika katika makao makuu ya ofisi hizo zilizopo Mlimani City jijini Dar es Salaam mbele ya waandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kusaini mkataba huo mpya, Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Vodacom, Kelvin Twissa, alisema kampuni yao inafurahia kuendelea kuwa sehemu ya udhamini ya Ligi Kuu Tanzania Bara, mafanikio ya timu bora na kufanya vizuri katika michuano ya kimataifa inatokana na kuwa na ligi bora ambayo inadhaminiwa na Vodacom.
Rais wa TFF, Jamal Malinzi amewashukuru kampuni ya Vodacom kwa kukubali kuendelea kuidhamini ligi kuu kwa kipindi kingine cha miaka mitatu (3) na kuongeza sehemu ya udhamini wao kwa asilimia 40. Kwa mwaka mkataba huo ambao utamalizika mwaka 2018, utakuwa na thamani ya Sh bilioni 2.3, baada ya ule wa awali kuwa wa thamani ya Sh bilioni 1.6 kwa kipindi hicho, na ulimalizika Julai mosi mwaka huu.
Kwa kusoma habari hii zaidi Bonyeza hapa :
No comments:
Post a Comment