SHAMBA LA BIBI

SHAMBA LA BIBI

Monday, 31 August 2015

JE WAJUA KUWA TANZANIA INA JUMLA YA WAGOMBEA 8 KATIKA NAFASI YA URAISI MWAKA HUU 2015...!? SOMA HAPA...


KIPIMO HURU KWA MTANZANIA MZALENDO:

Tukiwa tunaelekea Oktoba 25, katika hawa wagombea nane wa urais, tuambie wewe yupi amekushawishi kumpa kura yako?

A: Magufuli (CCM)
B: Mghwira (ACT)
C: Lowassa (CHADEMA)
D: Lyimo (TLP)
E: Chief Yemba (ADC)
F: Kasambala (NRA)
G: Rungwe (CHAUMA)
H: Dovutwa (UPDP)

Wednesday, 26 August 2015

MANCHESTER UNITED YAUA UGENINI, YAPITA

Wachezaji wa Manchester United wakifurahi


Katika muendelezo wa mechi za mkondo wa pili kufuzu kwenye mashindano ya klabu bingwa barani Ulaya, usiku wa kuamkia leo timu kadhaa zilishuka dimbani kutafuta tiketi ya kuingia katika hatua ya makundi.

 

Manchester Utd imefanikiwa kusonga mbele kwa kishindo baada ya kuibuka na ushindi wa bao 4-0 dhidi ya Club Brugge na kufanya matokeo kuwa 7-1, katika mikondo yote miwili.

 

Katika mchezo huo nahodha Wayne Rooney alidhihirisha kuwa bado yupo vizuri katika kucheka na nyavu, baada kufunga mara tatu.

 

Droo ya makundi ya ligi hiyo, inatarajiwa kufanyika leo hii.



Matokeo mengine Champions League:

UKAWA WAKATALIWA KUFANYA KAMPENI VIWANJA VYA JANGWANI JUMAMOSI. SOMA HAPA ...





MANCHESTER UNITED: TUTASHINDA LEO DHIDI YA CLUB BRUGGE!

Leo usiku michuano ya UEFA Champion League inaendelea tena huku ikutanisha miamba miwili ya soka barani humo, Manchester United ya Uingereza na Club Brugge kutoka nchini Ubelgiji.

 

Ikumbukwe mechi ya awali iliyopigwa katika uwanja wa Old Trafford jijini Manchester, 

vijana wa Luis Van Gaal (Manchester United) walishinda 3-1.


Una uhahisi timu ya United itafuzu hatua ya michuano ya Champions League?

Tabiri matokeo ya mchezo huu unaochezwa usiku wa leo huko Ubelgiji.

Tuesday, 25 August 2015

EDWARD NGOYAI LOWASSA ATOA KAULI HII MUDA HUU. AZIDI KUWAPA WAKATI MGUMU WAPINZANI WAKE... ISIKIE HAPA

"Uongozi usioyafahamu matatizo ya Watanzania kiundani hauna uhalali wa kuelezea suluhisho la matatizo hayo. 

 

Tumechoshwa na aina ya uongozi wa kuletewa ripoti maofisini, na Leo tumeendeleza ziara ya kuwatembelea wananchi na kusikia kero zao Za msingi. 

 

Tukutane Jangwani Jumamosi hii ya tarehe 28.8.2015 tuweze kuwaeleza namna tulivyojipanga kufanya ukombozi wa kiuchumi. Tuko Tayari kwa mabadiliko"

-Edward Ngoyai Lowassa

 



 


MGOMBEA WA URAIS KWA TIKETI YA CHADEMA EDWARD LOWASSA



Je una mtazamo gani mwanakwetu juu ya tukio hilo ...!?

SIKIA HII: KITENDO KAMA CHA LOWASSA KUPANDA DALADALA NA KUSHTUKIZA WANANCHI NI MARUFUKU- KOVA

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limepiga marufuku wagombea urais kufanya vitendo vinavyoweza kuhatarisha usalama wa wananchi.

 

Akiongea leo Jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Kanda hiyo Suleiman Kova ametolea mfano kitendo cha jana cha mgombea urais wa Chadema Mhe. Edward Lowassa cha kufanya ziara ya kushtukiza kwa wananchi na kupanda daladala.

 

Amesema ziara hiyo ya Mhe. Lowassa na mgombea mwenza wake Juma Duni Haji walitembelea Gogo la Mboto, ingeweza kuhatarisha usalama wa wananchi kwa kuwa watu wengi walikusanyika na wengine kuacha kazi zao.

BAADA YA BAADHI YA MASHABIKI KUMSHAMBULIA KWA MANENO, JB ASEMA HAYA

King Majuto na Jb
Kufuatia kitendo baadhi ya mashabiki kumshabulia kwa maneno makali staa wa Bongo Movies, JB kwa kuonyesha mapenzi yake kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kuelekea uchaguzi wa mwaka huu, JB amefunguka haya kwenye ukurasa wake mtandaoni kuwataka wabadilike kimtazamo.

Hakuna kitu muhimu kwenye maisha kama furaha....lakini furaha ina ambatana na kufanya mambo ambayo moyo wako unapenda bila kuvunja sheria.
Kuishi maisha ya kuogopa kitu unachopenda kwa sababu ya watu ni kuinyima furaha roho yako...watanzania wenzangu tuanze tabia ya kuheshimu maamuzi ya wenzetu.
Angalia hata kwenye mahusiano yetu watu wakiachana ni uhasama..kisa hatukubali kuwa mwenzako moyo wake uko kwingine.
Eti lazima akupende ww tu..haa...kwenye siasa ndio usiseme mtu akipenda upande mwingine ashakuwa adui.Aaah tubadilike.....sambaza upendo..+255 kwanza.

MSIMAMO LIGI KUU UINGEREZA (EPL) MPAKA KUFIKIA LEO TAREHE 25/08/2015



Nini maoni yako rafiki...!?

SIKIA HII: CCM YASHINDA MAJIMBO MATANO KABLA YA KUFIKA OCTOBAR, 25

Deo Filikunjombe

Kwa ufupi:

 

January Makamba
Jenister Mhagama

Chanzo: MCL


Niandikie mtazamo wako shwahiba wangu..., jamaa wanapita kiulaiiini kama vile....   !!!

Monday, 24 August 2015

WASOMI WAMSHUKIA MKAPA KWA KAULI ZA KUUDHI

Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa akihutubia umati wa wafuasi wa CCM waliohudhuria ufunguzi wa kampeni za mgombea urais wa chama hicho uliofanyika katika Viwanja vya Jangwa, Dar es Salaam juzi.

LOWASSA AIBUA STAILI MPYA YA KAMPENI

Mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa (kushoto) akilipa nauli kwa kondakta wa daladala iliyokuwa ikitoka Gongo la Mboto kuelekea Chanika alipofanya ziara ya kusikiliza kero zinazowakabili watumiaji wa usafiri wa umma, madereva na makondakta, Dar es Salaam jana.

MAGUFULI AFUNGUA PAZIA LA KAMPENI, ATAJA VIPAUMBELE 25

Mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli akihutubia wafuasi wa chama hicho waliofurika katika Viwanja vya Jangwani, Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa kampeni za chama hicho jana. Picha na Edwin Mjwahuzi