FLOYD MAYWEATHER NOMA, AMDUNDA ANDRE BERTO JANA USIKU..., SOMA HAPA
Andre Berto akipigana na Floyd Mayweather Las Vegas
Bingwa wa ndondi katika uzani wa
welter duniani Floyd Mayweather ameshinda pigano lake la 49 mfululizo
kwa alama baada ya kumlemea Andre Berto mjini Las Vegas.
Berto
alikuwa moto lakini Mayweather, aliyekuwa akitetea mataji ya WBC na WBA
katika uzani wa welter, alijikinga sana na kukwepa ngumi za Mmarekani
huyo mwenzake.
Mayweather, 38, alizawadiwa alama 120-108, 118-110
na 117-111 kwenye pigano hilo lililoandaliwa ukumbi wa MGM Grand usiku
wa kuamkia Jumapili.
Mayweather amesisitiza kuwa hilo litakuwa
pigano lake la mwisho, lakini ikizingatiwa kwamba amefikia rekodi ya
Rocky Marciano ya kupambana na kushinda mapigano 49-0, huenda akaamua
kuongeza.
"Maisha yangu ya uchezaji yamefikia kikomo, hilo ni
rasmi,” alisema Mayweather ambaye sasa ni bingwa wa ndondi katika
vitengo vitatu tofauti vya uzani.
Bondia huyo anachukuliwa sana na wengi kuwa stadi zaidi katika kizazi chake.
"Lazima
ujue wakati wa kuacha. Sasa nakaribia umri wa miaka 40. Sijabaki na
chochote cha kuthibitisha kwa ulimwengu wa masumbwi. Sasa nataka tu
kufurahia maisha na familia yangu.”
Berto, 32, ni bingwa mara
mbili wa dunia uzani wa welter na aliingia kwenye pambano hilo akiwa
amewahi kupoteza mara tatu pekee katika mapigano 33 ya kulipwa
aliyoshiriki.
Mayweather aliyekuwa akipigania ubingwa wa dunia mara ya 26 hajawahi kushindwa tangu 1996.
Iwapo ataamua kutostaafu, wengi wanatarajia huenda akaamua kukabiliana tena na Manny Pacquiao mwaka ujao.
Ukumbi
mpya wa MGM utafunguliwa Aprili na pambano dhidi ya Pacquiao, ambaye
Mayweather alimshinda Mei kwenye pigano lenye pesa nyingi zaidi katika
historia, huenda likamvutia sana.
Aidha, anaweza pia akashawishika kukutana na mshindi wa pigano la Novemba 21 kati ya Miguel Cotto na Saul Alvarez.
Nini maoni yako mdau.., ni kwamba huyu jamaa (Floyd) ameshindikana au...!?
No comments:
Post a Comment