SHAMBA LA BIBI

SHAMBA LA BIBI

Sunday, 27 September 2015

BASATA KURUDISHA HADHI YA MUZIKI WA REGGAE. SOMA HAPA KWA HABARI ZAIDI...

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa kushirikiana na Kampuni ya Reggae Production House iliyo chini ya Msanii Mkongwe wa reggae Innocent Nganyagwa limeandaa programu maalum kwa ajili ya kurudisha hadhi ya muziki wa reggae nchini.

 

Programu hiyo ambayo itafanyika makao makuu ya BASATA yaliyoko Ilala Sharif Shamba jijini Dar es Salaam Jumatatu ya Tarehe 28/09/2015 kuanzia saa 4:00 hadi saa 6:30 Mchana kupitia Programu ya Jukwaa la Sanaa, itakuwa mahsusi kwa ajili ya kuurudisha muziki wa reggae jukwaani, kujadili mwelekeo wa muziki huu na kuja na mikakati bora ya kuurudishia hadhi yake. 

 

Ieleweke kwamba katika siku za karibuni muziki huu wa reggae umekuwa umeganda na kutokupiga hatua kubwa hali ambayo imewafanya wadau wa muziki kukosa burudani ambayo wamekuwa wakiipata huko nyuma kupitia kwa wasanii wakongwe kama Innocent Nganyagwa, Innocent Garinoma, Justine Kalikawe na wengineo.

 

Changamoto kubwa si tu ni muziki huu kutochezwa kwenye vyombo vya habari bali pia kuna changamoto ya wasanii wenyewe kutokubadilika na kutengeneza muziki unaokwenda sambamba na soko pia hitaji la mashabiki. 

 

Ni nia ya BASATA kuona wasanii na wadau wote wa muziki nchini wanahudhuria programu hii mahsusi kwa lengo la kujadiliana kwa pamoja hatma ya muziki wa reggae, kupata historia ya jinsi ulivyokuwa huko nyuma, kutazama na kuburudika Jukwaani na muziki wa mmoja wa wasanii wakongwe wa muziki huu.

 

BASATA linaamini kwamba baada ya programu hii wasanii wa reggae na wadau kwa ujumla watakuwa na mwanzo mpya katika kurudisha hadhi ya muziki wa reggae nchini na kuhakikisha unaendelea kudumu.

 

Sanaa ni Kazi, tuikuze, tuitunze na kuithamini

 

 

IMETOLEWA NA KITENGO CHA HABARI BASATA

JE CATALONIA ITAJITENGA NA UHISPANIA...!? SOMA HAPA...

Zaidi ya watu milioni tano wamejiandikisha kupiga kura .

Watu wa eneo la Catalonia nchini Uhispania wameanza kupiga kura katika uchaguzi uunaotazamwa kuwa mtihani mkubwa wa kuunga mkono Uhuru wa eneo hilo tajiri.

 

Pia mbali na utajili wa eneo hilo pia kuna vipaji vingi vya timu ya mpira wa miguu vinavyochezea timu ya Taifa hilo lakini pia klabu ya Barcelona ambayo na yenyewe ipo eneo hilo.

 

Wanachama wa vyama vya Catalan, wanaotaka kujitenga na ambao wanaongoza katika kura ya maoni wanasema kuwa ushindi utavipa vyama vyao uwezo wa kutangaza kwa kauli moja uhuru wao.

 

Je Catalonia itajitenga na Uhispania ?

 Serikali ya Uhispania ambayo inakataa kata kata kukubalia shughuli hizo za upigaji wa kura ya maoni kuhusiana na swala hilo imetaja kura hiyo ya maoni kama upuzi mtupu.

 

Kocha wa Bayern Munich Pep Guardiola akipiga kura

 

 

Uchaguzi huo unaonekana kama swala muhimu katika historia ya hivi punde ya Uhispania.

BASATA LATAKA KUONDOLEWA/KUSITISHWA MARA MOJA KUCHEZWA KWA NYIMBO ZOTE ZENYE KUKENGEUKA MAADILI, SHERIA NA TARATIBU. SOMA HAPA...

Katibu Mtendaji wa BAsata, Bw. Mngereza

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) linawaagiza wasanii, wamiliki na waendeshaji wa wavuti, tovuti na vyombo vya habari hususan radio na runinga kuondoa na kuacha mara moja kurusha au kutangaza au kucheza nyimbo zote zenye maudhui ya kashfa, matusi, kejeli, udhalilishaji ambazo zinahatarisha kuigawa jamii ya kitanzania katika misingi yoyote hasa katika kipindi hiki Taifa linapoendelea na kampeni za kisiasa na kujiandaa na uchaguzi mkuu.

 


Kwa mujibu wa kifungu namba 118 (a-d) cha Sheria ya Bunge namba 9 ya Mawasiliano ya Mtandao ya mwaka 2010 ni marufuku kwa njia yoyote kwa mtu au chombo chochote kutengeneza, kuzalisha, kusambaza au kutangaza ujumbe ambao una mlengo wa matusi, dharau, uzushi au jinai kwa lengo la kutukana, kutisha, kusumbua au kushusha hadhi ya mtu mwingine.

 


Aidha, Sheria ya Bunge namba 4 ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015 kifungu cha 45 (1) (a-c) kinatoa mamlaka kwa taasisi au mtu yeyote anayebaini uvunjifu wa Sheria katika mitandao kutoa notisi kwa yeyote yule anayesambaza au kutangaza ujumbe au maudhui yanayovunja sheria za nchi kuacha mara moja au vinginevyo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya yeyote anayekaidi.

 


Ni kwa msingi huu, BASATA linawaagiza wasanii, wamiliki wa wavuti, tovuti na wale wenye akaunti kwenye mitandao ya kijamii kama sound cloud, U-Tube, ITunes nk. kuondoa ndani ya siku saba (7) kuanzia siku ya kwanza ya taarifa hii nyimbo zote zinazokengeuka maadili na kubeba mlengo wa matusi, kashfa, kejeli na udhalilishaji wa watu wa kada mbalimbali wakiwemo viongozi wa kisiasa na kitaifa.

 


Aidha, BASATA linawakumbusha tena Wasanii wote nchini kuacha mara moja kubuni na kutengeneza kazi za Sanaa zenye kuashiria kuigawa jamii katika misingi yoyote ya kibaguzi na zaidi kutumia Sanaa kubomoa jamii badala ya kuijenga.

 


BASATA linawasisitiza wamiliki wa vyombo vya habari hususan radio na runinga pia watangazaji na Ma DJs kuhakikisha hawawi chanzo cha kusambaza maudhui yoyote ya Sanaa yenye mlengo wa kuibua chuki, matusi, kashfa na mgawanyiko wa Taifa.

 


BASATA kwa mamlaka yake chini ya Sheria namba 23 ya mwaka 1984 na yale ya Sheria ya Mawasiliano ya Posta na Mitandao ya mwaka 2010 na ile ya Makosa ya mitandao ya mwaka 2015 kwa kushirikiana na vyombo vya dola halitasita kuchukua hatua kali za kisheria na kinidhamu kwa wasanii, wamiliki wa wavuti, tovuti na vyombo vya habari ambavyo vitaendelea kutangaza na kusambaza nyimbo zenye mwelekeo wa kuhatarisha usalama, umoja na mshikamano wa Taifa.

 


BASATA likiwa ni msimamizi na mratibu wa sekta ya Sanaa nchini linatambua kwamba Sanaa ikitumiwa kwa ukengeufu inaweza kuwa chanzo kikuu cha machafuko, mivurugano na kupotea kwa amani nchini. Hivyo umakini unahitajika miongoni mwa wasanii katika kuzingatia weledi, maadili, uzalendo kwa taifa na kuitumia Sanaa kama chombo cha kujenga jamii yenye kuzingatia maadili.  

 


SANAA NI KAZI TUIKUZE, TUILINDE NA KUITHAMINI

 

 


 


Godfrey L. Mngereza 

 


KATIBU MTENDAJI, BASATA


 

MANCHESTER UNITED YAONGOZA LIGI YA EPL. SOMA HAPA...


Nini maoni yako mdau kutokana na huo msimamo na unaizungumziaje nafasi ya Man U...!?

Saturday, 26 September 2015

PATA MATOKEA YOTE YA MECHI MUHIMU ZA EPL ZILIZOPIGWA JANA. INGIA HAPA...



Wakati Chelsea wakikabwa koo..., Arsenal yatembeza kichapo cha mbwa mwitu ugenini..!




Manchester United nayo ilimchinja Sunderland bila huruma...!








Manchester City nae aliangukia pua baada ya kukubali kichapo cha 4-1 kutoka kwa Tottenham Hotspur





MAMBO MUHIMU AMBAYO LAZIMA UYAJUE KABLA YA MECHI YA SIMBA VS YANGA




Leo ni siku ambayo ilikuwa ikisubiriwa sana na mashabiki wengi wa soka la Tanzania, leo ndio siku ambayo unapigwa mtanange wa Dar es Salaam Darby (Yanga vs Simba) mechi hii inatajwa kuwa miongoni mwa Derby kubwa barani Afrika lakini ikiwa ni Derby yenye upinzani mkubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Simba na Yanga zinakutana leo kwenye raundi ya nne ya VPL lakini ikiwa ni mechi ya kwanza inayozikutanisha timu hizo msimu huu, hapa chini nimekuwekea vitu muhimu unavyotakiwa kuvijua kabla ya mechi haijapigwa ili wakati wa mchezo utapofika unakuwa unajua vizuri nini kinaendelea.

 

 

Matokeo ya timu zote msimu huu mpaka sasa

Baada ya mechi tatu kuwa zimechezwa hadi sasa, timu zote zimeshinda michezo yote mitatu Simba imeshinda mechi zake dhidi ya African Sports na Mgambo JKT ugenini kwenye uwanja wa Mkwakwani, Tanga mechi yao ya tatu walishinda wakiwa kwenye uwanja wa taifa dhidi ya Kagera Sugar. Yanga mechi zao zote wameshinda wakiwa kwenye uwanja wa taifa dhidi ya Coatal Union, Tanzania Prisons na JKT Ruvu.

 

 

Vita ya Hamisi Kiiza vs Amis Tambwe

Hawa ni washambuliaji wawili ambao leo watakuwa wakicheza dhidi ya vilabu vyao vya zamani. Kiiza alikuwa Yanga kwasasa yupo Simba wakati Tambwe alikuwa Simba na sasa yupo Yanga na wote kwa pamoja wamekuwa na moto wa ajabu katika kutupia kambani msimu huu.

 

 

 

Kiiza

Mpaka sasa anaongoza kwa kutupia nyavuni akiwa amefunga bao tano baada ya kufunga kwenye mechi ya kwanza bao moja, mechi ya pili bao moja na mechi ya tatu bao tatu na hii ikiwa ni hat-trick ya kwanza kwa msimu huu lakini ikiwa ni hat-trick yake ya kwanza pia akiwa Msimbazi.

 

Tambwe

Amefunga jumla ya bao tatu hadi sasa. Alifunga bao moja kwenye mechi ya kwanza, halafu mechi ya tatu akatupia mbili dhidi ya JKT Ruvu wakati Yanga ilipoibuka na ushindi wa goli 4-1.

 

 

Mtiririko wa matokeo

 

Yanga

 

Walianza kwa ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Coasta Union, wakapata ushindi wa goli 3-0 dhidi ya Tanzania Prisons na mechi ya tatu wakashinda kwa goli 4-1 dhidi ya JKT Ruvu. Leo wanakutana na ‘mnyama’ hii ina maana kama wanaendelea kwa mfululizo huo wataibuka na goli tano.

 

 

 

Simba

 

Walianza kwa ushindi wa goli 1-0 dhidi ya African Sports kwenye mechi ya kwanza, mechi ya pili wakashinda kwa goli 2-0 dhidi ya Mgambo JKT na mechi ya tatu wakaibuka na ushindi wa goli 3-1 dhidi ya Kagera Sugar. Kama wataendelea na mfululizo huohuo inamaana leo watafunga bao nne.

 

 

 

Magoli ya kufungwa

 

Kila timu imeruhusu goli moja kwenye mchezo wake wa tatu, timu zote zimefungwa kwenye uwanja wa taifa ambao zinautumia kama uwanja wao wa nyumbani na kila timu imefungwa kwenye mchezo iliopata ushindi mkubwa.

 

Yanga

 

 Imefungwa goli moja wakati ilioibuka na ushindi wa goli 4-1 dhidi ya JKT Ruvu mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa taifa. Yanga wamefunga magoli tisa kwenye mechi tatu walizocheza.

 

 

 

Simba

 

Ilifungwa goli moja kwenye ushindi wake mkubwa msimu huu hadi sasa ilipoifunga Kagera Sugar kwa goli 3-1 kwenye uwanja wa taifa wakati wao wakiwa wamefunga jumla ya magoli sita hadi sasa.

 

 

 

Historia ya timu hizo kwenye mchezo wa Dar es Salaam Derby

 

Timu hizi tayari zimekutana mara 79 kwenye mechi za ligi kuu Tanzania bara, mchezo wa leo utakuwa ni wa 80 huku ukiwa ni wakwanza kwenye msimu huu wa 2015/16.

 

Takwimu zinazungumaje?

 

Mabinwa watetezi wa ligi hiyo timu ya Yanga wanaongoza kwa kuwafunga watani zao Simba wakiwa wameshinda mechi 29 kati ya 79 wakati Simba wao wameifunga Yanga kwenye mechi 23 kati ya 79 huku mechi mechi 27 kati ya 79 zikiwa nisare.

 

Matokeo ya msimu uliopita

 

Kwenye mechi ya kwanza msimu uliopita timu hizo zilitoka sare lakini mechi ya pili (marudiano) Simba iliitandika Yanga kwa bao 1-0 lililofungwa na mshambuliaji wa Uganda Emanuel Okwi.

 

Maswali mawili ya kujiuliza kabla ya mchezo wa leo

 

1. Je, Yanga ambao ni mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara watalipa kisasi cha kufungwa mara kwa mara siku za hivi karibuni au Simba wataendelea kupeleka kilio Jangwani?

 

2. Je, ni nani kati ya Kiiza na Tambwe atakaepeleka kilio kwenye timu yake ya zamani?


MORINHO AMKEJELI WENGER

Mourinho

Mkufunzi wa kilabu ya Chelsea Jose Mourinho amemkosoa tena mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger akimtaja kuwa mfalme anayeongoza bila presha.

 

Wenger alidhani kwamba uchokozi wa Diego Costa ndio uliosababisha Gabriel Paulista kupewa kadi nyekundu katika mechi kati ya timu hizo mbili iliochezwa wikiendi iliopita.


Mourinho na Wenger

Mourinho bila kumtaja mtu yeyote alisema:''Anaweza kuzungumza kuhusu marefa,kuwasukuma watu,unaweza kulia kuanzia asaubuhi hadi jioni lakini hakuna chochote kitakachofanyika.Hawezi kutoa matokeo mazuri lakini bado anaendelea kuwa mfalme''.

 

Wawili hao wamekuwa na uadui mkubwa huku Mourinho akimwita Wenger kuwa maalum bila mafanikio.

Tuesday, 22 September 2015

BEI YA DAWA YA UKIMWI YAPANDISHWA 5000%. SOMA HABARI HII KWA KINA HAPA...

Bei ya dawa ya ukimwi yapandishwa 5000% 


Kampuni moja ya kutengeza madawa imelazimika kujitetea vikali baada ya kupandisha gharama ya dawa ya Ukimwi kwa asilimia 5,000.


Hii inamaanisha kuwa bei ya tembe moja ya dawa inayotumika kupunguza makali ya ukimwi itapanda kutoka dola $13.50 hadi $750.


Kampuni hiyo inayoitwa Turing Pharmaceuticals imelaumiwa na washika dau wa maswala ya Ukimwi kwa kuongeza bei ya dawa hiyo ya Daraprim ambayo imekuwa mstari wa mbele katika kuimarisha uwezo wa mwili wa mgonjwa aliyeathirika kupigana na maambukizi mapya.


Turing Pharmaceuticals ilinunua hati miliki ya dawa hiyo ya Daraprim mwezi uliopita Agosti.


Mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo Martin Shkreli amenukuliwa akisema kuwa faida itakapatikana baada ya mauzo ya dawa hiyo itasaidia kugharamia utafiti wa dawa mpya na zenye ubora zaidi.


Tembe moja ya dawa hiyo ya Daraprim inagharimu dola moja pekee kutengeneza.


Mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo Martin Shkreli amenukuliwa akisema kuwa faida itakapatikana baada ya mauzo ya dawa hiyo itasaidia kugharamia utafiti wa dawa mpya

Hata hivyo bwana Martin Shkreli anasema kuwa bei hiyo haijumuishi gharama ya kunadi dawa hiyo wala usambazaji wake ilihali gharama imeimarika maradufu katika miaka ya hivi punde.


''Katika siku za hivi punde dawa za kupunguza makali ya saratani zinagharimu dola laki moja (100,000) ilhali gharama yake asili inaweza kugharimu dola nusu milioni.


Daraprim inauzwa kwa bei nafuu zaidi ikilinganishwa na dawa zinazotibu magonjwa sawa.


Shkreli aliiambia runinga ya Bloomberg katika mahojiano ya kibinafsi.


Shkreli alimsuta mwandishi mmoja wa habari kupitia mtandao wa Kijamii akimuita kuwa ''mjinga'' kwa kutaka kujua kwanini kampuni yake ilikuwa inaongeza maradufu bei ya dawa hiyo muhimu katika vita dhidi ya Ukimwi haswa katika mataifa maskini duniani.


Tembe moja ya dawa inayotumika kupunguza makali ya ukimwi itapanda kutoka dola $13.50 hadi $750.

Daktari Wendy Armstrong kutoka muungano wa wauguzi nchini Marekani HIV Medicine Association amekashifu sababu zilizotolewa kwaajili ya nyongeza hiyo kubwa ya bei ya dawa hiyo.


Muaniaji tikiti cha urais wa chama cha Democratic Hillary Clinton ameonya kuwa serikali yake itachukua hatua kali dhidi ya makampuni yanayofaidi kutokana na msiba wa watu kwa kupandisha bei ya madawa maalum.


Chanzo: BBC Swahili



Nini maoni yako Mtanzania juu ya kupandishwa bei kwa dawa hii muhimu katika maisha ya mwanadamu hasa kutokana na janga hili la Ukimwi....!? 

Sunday, 13 September 2015

FLOYD MAYWEATHER NOMA, AMDUNDA ANDRE BERTO JANA USIKU..., SOMA HAPA

Andre Berto akipigana na Floyd Mayweather Las Vegas

Bingwa wa ndondi katika uzani wa welter duniani Floyd Mayweather ameshinda pigano lake la 49 mfululizo kwa alama baada ya kumlemea Andre Berto mjini Las Vegas.

 

Berto alikuwa moto lakini Mayweather, aliyekuwa akitetea mataji ya WBC na WBA katika uzani wa welter, alijikinga sana na kukwepa ngumi za Mmarekani huyo mwenzake.

 

Mayweather, 38, alizawadiwa alama 120-108, 118-110 na 117-111 kwenye pigano hilo lililoandaliwa ukumbi wa MGM Grand usiku wa kuamkia Jumapili.

 

Mayweather amesisitiza kuwa hilo litakuwa pigano lake la mwisho, lakini ikizingatiwa kwamba amefikia rekodi ya Rocky Marciano ya kupambana na kushinda mapigano 49-0, huenda akaamua kuongeza.

 

"Maisha yangu ya uchezaji yamefikia kikomo, hilo ni rasmi,” alisema Mayweather ambaye sasa ni bingwa wa ndondi katika vitengo vitatu tofauti vya uzani.

 

Bondia huyo anachukuliwa sana na wengi kuwa stadi zaidi katika kizazi chake.

 

"Lazima ujue wakati wa kuacha. Sasa nakaribia umri wa miaka 40. Sijabaki na chochote cha kuthibitisha kwa ulimwengu wa masumbwi. Sasa nataka tu kufurahia maisha na familia yangu.”

 

Berto, 32, ni bingwa mara mbili wa dunia uzani wa welter na aliingia kwenye pambano hilo akiwa amewahi kupoteza mara tatu pekee katika mapigano 33 ya kulipwa aliyoshiriki.

 

 

Mayweather aliyekuwa akipigania ubingwa wa dunia mara ya 26 hajawahi kushindwa tangu 1996.

 

Iwapo ataamua kutostaafu, wengi wanatarajia huenda akaamua kukabiliana tena na Manny Pacquiao mwaka ujao.

 

Ukumbi mpya wa MGM utafunguliwa Aprili na pambano dhidi ya Pacquiao, ambaye Mayweather alimshinda Mei kwenye pigano lenye pesa nyingi zaidi katika historia, huenda likamvutia sana.

 

Aidha, anaweza pia akashawishika kukutana na mshindi wa pigano la Novemba 21 kati ya Miguel Cotto na Saul Alvarez.

 

 

Nini maoni yako mdau.., ni kwamba huyu jamaa (Floyd) ameshindikana au...!?

MANCHESTER UNITED YAIPIGA KICHAPO CHA MBWA MWITU LIVERPOOL JANA...


Matokeo mengine ya EPL (English Primier League) haya hapa...


Monday, 7 September 2015

GWAJIMA KUJIBU MAPIGO YA DR. SLAA KESHO DAR...! SOMA HABARI HII HAPA...

Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima.

Askofu wa kanisa la ufufuo na uzima, Josephat Gwajima kesho anatarajia kujibu mapigo kuhusu tuhuma dhidi yake zilizotolewa na Katibu Mkuu wa zamani wa Chadema Dr. Willibrod Slaa ambaye hivi karibuni alimweleza kuwa ni mshenga wa Edward Lowassa kwa viongozi wa Chadema.

 

 

 

 Chanzo: MCL

Sunday, 6 September 2015

PATA MATOKEO YA KOMBE LA MATAIFA YA AFRICA YA MECHI ZOTE MUHIMU ZILIZOCHEZWA WIKIEND HII...


Matokeo ya baadhi ya mechi za kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika.

Djibouti 0-2 Togo
Namibia 0-2 Senegal
Comoros 0-1 Uganda
Burundi 2-0 Niger
Rwanda 0-1 Ghana
Tanzania 0-0 Nigeria
Seychelles 1-1 Ethiopia

Wednesday, 2 September 2015

WANAJESHI 50 WA AFRICAN UNION (AU) WAUWAWA NCHINI SOMALIA

Wapiganaji wa Al shabaab

Takriban wanajeshi 50, wa kutunza amani wa Muungano wa Afrika, wengi wao kutoka Uganda, wanasadikika kuuawa kwenye shambulio, lililofanywa siku ya Jumanne na wapiganaji wa Al shabaab, katika kambi ya Jannale, ulioko umbali wa kilomita 115 Kusini mwa mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.

 

Wakaazi wa wilaya hiyo wamethibitisha kuwa kambi hiyo ilishambuliwa na wapiganaji hao wa Al Shabaab.

 

Wanasema wameonya helicopta za kijeshi mapema hii leo ikiwatafuta wanajeshi waliopotea katika maeneo ya mashambani na pia kuwauliza wakaazi hao ikiwa wamewaona wanajeshi wa AU wakiwa hai au wakiwa wameuawa.

 

Miili tatu ilipatikana karibu na kijiji hicho, baada ya watu hao kuzama ndani ya mto wakati wa makabiliano makali ya risasi.

Wanajeshi wa AU nchini Somalia

 

Wanasema kuwa waliwapata wanajeshi kadhaa wakiwa hai na wengine wakiwa wameuawa.

 

Wanajeshi hao wa AU wanakabiliwa na wakati mgumu katika operesheni hiyo kwa sababu daraja inayounganisha mji huo uliharibiwa kwa mabomu hiyo jana.

 

Hali imeanza kutulia mjini humo lakini wakaazi wanaamini kuwa zaidi ya wanajeshi 40 hawajulikani waliko.

 

Makao makuu ya kikosi cha Muungano wa Afrika nchini Somalia, AMISOM, imethibitisha kuwa waliwapoteza wanajeshi akdhaa kutoka Uganda lakini idadi yao haijulikani.

Wanajeshi wa AMISOM



Chanzo: BBC Swahili

DIRISHA LA USAJILI LAFUNGWA UINGEREZA, FAHAMU NANI AMEKWENDA WAPI NA NANI AMETOKA WAPI... SOMA HAPA

Anthony Martial mchezaji mpya wa Manchester United

Vilabu nchini Uingereza, vilivunja rekodi ya kutumia pesa nyingi zaidi katika historia ya Ligi ya Premier majira ya joto huku pesa zilizotumiwa na vilabu hivyo katika mwaka mmoja zikifika £1bn kwa mara ya kwanza.

Katika kipindi cha kuhama wachezaji kilichomalizika siku ya Jumanne, vilabu vilitumia £870m, 4% juu ya rekodi iliyowekwa mwaka uliopita.


Ukiongeza £130m zilizotumiwa na vilabu hivyo dirisha fupi Januari, kiasi hicho kinafikia £1bn.

Kilabu ya Manchester City ilitumia pesa nyingi zaidi, ikinunua wachezaji wawili bei ghali zaidi, £55m kwa Kevin De Bruyne kutoka Wolfsburg na £49m kwa Raheem Sterling kutoka Liverpool.

 

Usajili wa Manchester United wa £36m kumchukua mchezaji wa Monaco, Anthony Martial, ulikuwa wa juu zaidi siku ya mwisho ya kuhama wachezaji.

 

Gharama yake inaweza kupanda hadi £58m ukiongeza vikolezo vingine.

Kevin De Bruyne

 

Tangu kuanzishwa kwa mfumo wa kuwepo kwa awamu ya kuhama wachezaji 2002, jumla ya pesa zilizotumiwa imezidi £7.3bn, zaidi ya 80% ya kiasi hicho zikitumiwa majira ya joto, kwa mujibu wa wadadisi wa kifedha wa Deloitte.

 

Kuhamia kwa Kevin De Bruyne, Manchester City, ndiko kulikokuwa ghali zaidi sokoni.

 

Manchester City walivunja rekodi ya klabu hiyo mara mbili awamu iliyopita ya usajili kwa kuwanunua De Bruyne na Sterling na kuwafanya kuwa klabu iliyotumia pesa nyingi zaidi kwa awamu moja nchini Uingereza.

 

Jumla ya pesa walizotumia ya takriban £160m, inazidi takriban £150m walizotumia Manchester United, majira ya joto 2014, wachezaji wengine waliowanunua wakiwa Fabian Delph, Patrick Roberts na Nicolas Otamendi.

Nicolas Otamendi

 

Viongozi hao wa sasa wa Ligi ya Premia walipata afueni majira ya sasa ya joto baada ya kuondolewa vikwazo vya matumizi ya pesa walipotimiza lengo walilowekewa chini ya sheria mpya ya haki na usawa.

City walikuwa wamewekewa kiwango cha juu cha matumizi cha £49 mwaka 2014 na walitozwa pia faini ya £16.3m kwa kukiuka kanuni za Uefa.

 

Vilabu vinne vya Ligi ya Premier, vinavyoshiriki Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya msimu huu Manchester City, Manchester United, Chelsea na Arsenal vilitumia kwa jumla takriban £340m, ikiwa ni karibu 40% ya jumla ya pesa zilizotumiwa na klabu za Ligi ya Premier, kununua wachezaji.

 

Kununuliwa kwa Martial mwenye umri wa miaka 19, Everton kumnunua mlinzi wa Argentina Ramiro Funes Mori, kwa £9.5m na Papy Djilobodji kununuliwa £4m na Chelsea kutoka Nantes, siku ya Jumanne kuliwezesha awamu hii ya usajili kupita £835m zilizotumiwa mwaka jana.

Papy Djiboloboj

 

Liverpool wametumia pesa zaidi kuwasajili wachezaji saba, Christian Benteke (£32.5m), Roberto Firmino (£29m) na Nathaniel Clyne (£12m) wakiwa ndio ghali zaidi.

 

Manchester United pia wamekuwa mbioni, wakitumia £139m kununua Martial, Memphis Depay, Matteo Darmian, Bastian Schweinsteiger na Morgan Schneiderlin, huku Chelsea wakisubiri hadi dakika za mwisho kununua wachezaji wa thamani, wakiwachukua Pedro, Baba Rahman na Djilobodji.

 

Kilabu iliyopandishwa daraja majuzi ya Watford ndiyo iliyonunua wachezaji wengi zaidi ligini, ikiwapata wachezaji 15 wapya.

bastian schweinsteiger and morgan schneiderlin