SHAMBA LA BIBI
Wednesday, 28 December 2016
Friday, 23 September 2016
DANGOTE KUINUNUA ARSENAL KATIKA KIPINDI CHA MIAKA 4
![]() |
Mtu tajiri barani Afrika kuinunua Arsenal |
Aliko Dangote, mtu tajiri zaidi barani Afrika,ana mpango wa kuinunua klabu ya Arsenal kutoka nchini Uingereza katika kipindi cha miaka minne.
Dangote ambaye ni raia wa Nigeria ana thamani ya dola bilioni 10.9,kulingana na orodha ya watu tajiri duniani iliotolewa na runinga ya Bloomberg mjini New York siku ya Jumatano, alitangaza nia yake ya kukinunua klabu hicho mwaka uliopita.
Alisema kuwa anasubiri biashara zake kuimarika pamoja na uwekezaji wake wa ujenzi wa bomba la gesi na kiwanda cha kusafisha mafuta kabla ya kukinunua klabu hicho.
''Hakuna tatizo kwamba atakinunua klabu hicho'' na si tatizo la fedha ,alisema Dangote katika mahojiano na runinga ya Bloomberg .
![]() |
Arsenal |
''Pengine miaka mitatau au mine.Swala ni kwamba tunachangamoto nyingi.Ninahitajika kukabiliana nazo mwanzo baadaye nitaangazia swala la ununuzi huo''.
Dangote ambaye ni shabiki mkubwa wa Arsenal amepoteza kiasia cha dola bilioni 4.4 mwaka huu kutokana na kushuka kwa thamani ya sarufi ya Nigeria.
Utajiri wake mwingi upo katika kiwanda cha simiti cha mjini Lagos.
Iwapo atainunua timu hiyo basi atakuwa mtu wa kwanza kutoka barani Afrika kumiliki timu iliopo katika ligi kuu ya Uingereza.
Friday, 29 April 2016
BASATA KUAZIMISHA SIKU YA MUZIKI WA JAZZ DUNIANI
Baraza
la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa linalojishughulisha
na Elimu na Sayansi (UNESCO) litaungana na wasanii mbalimbali nchini na wadau
wa Sanaa kuazimisha siku ya muziki wa Jazz duniani ambayo kwa mara ya kwanza
itaazimishwa nchini Mei 2, 2016.
Maazimisho
hayo ambayo yatapambwa na burudani mbalimbali kutoka kwa Wasanii wa muziki wa
jazz hususan Band maarufu ya Das Jazz yanatarajiwa kufanyika kwenye Ukumbi wa
Baraza hilo ulioko Ofisi za BASATA Ilala Sharif Shamba jijini Dar es Salaam.
Sambamba
na burudani hizo, kutakuwa na mada mbalimbali zitakazowasilishwa na wadau wa
muziki huu wa jazz ambazo zitalenga kuamsha ari, thamani na ufahamu wa muziki
huu maarufu duniani miongoni mwa wasanii nchini.
Wawasilishaji
wa mada hizo pamoja na mada zao kwenye mabano ni pamoja na John Kitime
(Matumizi ya neno Jazz), Carola Kinasha (Uhusiano kati ya Elimu ya Muziki na
Jazz) na Kurwigira Mareges (Historia ya Muziki wa Jazz) na Masoud Masoud (Ujue
Muziki wa Jazz).
Mbali
na burudani na mada hizo kuhusu muziki huo wa Jazz kutakuwa na wageni waalikwa
kutoka kwenye balozi na vituo vya Utamaduni vya nchi mbalimbali zilizopo hapa
Tanzania.
BASATA
linatoa wito kwa wasanii na wadau wa muziki huu wa jazz kujitokeza kwa wingi
katika maadhimisho haya ambayo yatakuwa yakifanyika kila mwaka sambamba na
mataifa mengine duniani.
Sanaa ni kazi,
tuipende na kuithamini
Godfrey Mngereza
Katibu Mtendaji – BASATA
Friday, 25 March 2016
BARAZA LA SANAA LA TAIFA - BASATA: BASATA YAONYA KUMBI ZISIZOFUATA TARATIBU ZA VIBALI...
BARAZA LA SANAA LA TAIFA - BASATA: BASATA YAONYA KUMBI ZISIZOFUATA TARATIBU ZA VIBALI...: Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ambalo ni msimamizi wa sekta ya Sanaa na burudani nchini linawakumbusha wamiliki na waendeshaji wa ku...
Subscribe to:
Posts (Atom)