SHAMBA LA BIBI

SHAMBA LA BIBI

Friday, 17 February 2017

NYUMBANI NI NYUMBANI...!



Mwanamuziki maarufu nchini Snura Mushi alipokwenda kusalimia kwenye ofisi za BASATA leo hii. Mara ya mwisho kuonekana kwenye ofisi hizo ilikuwa ni kipindi kile alichotunga wimbo wake wa "Chura" ambao video yake ilileta ukakasi kwenye jamii.

 

 

Nini maoni yako...!?


Friday, 23 September 2016

DANGOTE KUINUNUA ARSENAL KATIKA KIPINDI CHA MIAKA 4

Mtu tajiri barani Afrika kuinunua Arsenal

Aliko Dangote, mtu tajiri zaidi barani Afrika,ana mpango wa kuinunua klabu ya Arsenal kutoka nchini Uingereza katika kipindi cha miaka minne.


Dangote ambaye ni raia wa Nigeria ana thamani ya dola bilioni 10.9,kulingana na orodha ya watu tajiri duniani iliotolewa na runinga ya Bloomberg mjini New York siku ya Jumatano, alitangaza nia yake ya kukinunua klabu hicho mwaka uliopita.

Alisema kuwa anasubiri biashara zake kuimarika pamoja na uwekezaji wake wa ujenzi wa bomba la gesi na kiwanda cha kusafisha mafuta kabla ya kukinunua klabu hicho.

''Hakuna tatizo kwamba atakinunua klabu hicho'' na si tatizo la fedha ,alisema Dangote katika mahojiano na runinga ya Bloomberg .

Arsenal

''Pengine miaka mitatau au mine.Swala ni kwamba tunachangamoto nyingi.Ninahitajika kukabiliana nazo mwanzo baadaye nitaangazia swala la ununuzi huo''.

Dangote ambaye ni shabiki mkubwa wa Arsenal amepoteza kiasia cha dola bilioni 4.4 mwaka huu kutokana na kushuka kwa thamani ya sarufi ya Nigeria.

Utajiri wake mwingi upo katika kiwanda cha simiti cha mjini Lagos.

Iwapo atainunua timu hiyo basi atakuwa mtu wa kwanza kutoka barani Afrika kumiliki timu iliopo katika ligi kuu ya Uingereza.

 

Friday, 29 April 2016

BASATA KUAZIMISHA SIKU YA MUZIKI WA JAZZ DUNIANI




Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa linalojishughulisha na Elimu na Sayansi (UNESCO) litaungana na wasanii mbalimbali nchini na wadau wa Sanaa kuazimisha siku ya muziki wa Jazz duniani ambayo kwa mara ya kwanza itaazimishwa nchini Mei 2, 2016.

Maazimisho hayo ambayo yatapambwa na burudani mbalimbali kutoka kwa Wasanii wa muziki wa jazz hususan Band maarufu ya Das Jazz yanatarajiwa kufanyika kwenye Ukumbi wa Baraza hilo ulioko Ofisi za BASATA Ilala Sharif Shamba jijini Dar es Salaam.

Sambamba na burudani hizo, kutakuwa na mada mbalimbali zitakazowasilishwa na wadau wa muziki huu wa jazz ambazo zitalenga kuamsha ari, thamani na ufahamu wa muziki huu maarufu duniani miongoni mwa wasanii nchini.

Wawasilishaji wa mada hizo pamoja na mada zao kwenye mabano ni pamoja na John Kitime (Matumizi ya neno Jazz), Carola Kinasha (Uhusiano kati ya Elimu ya Muziki na Jazz) na Kurwigira Mareges (Historia ya Muziki wa Jazz) na Masoud Masoud (Ujue Muziki wa Jazz).

Mbali na burudani na mada hizo kuhusu muziki huo wa Jazz kutakuwa na wageni waalikwa kutoka kwenye balozi na vituo vya Utamaduni vya nchi mbalimbali zilizopo hapa Tanzania.
              
BASATA linatoa wito kwa wasanii na wadau wa muziki huu wa jazz kujitokeza kwa wingi katika maadhimisho haya ambayo yatakuwa yakifanyika kila mwaka sambamba na mataifa mengine duniani. 

Sanaa ni kazi, tuipende na kuithamini


Godfrey Mngereza
Katibu Mtendaji – BASATA

KUADIMISHA SIKU YA MUZIKI WA JAZZ DUNIANI. KITAIFA ITAFANYIKA DAR ES SALAAM KATIKA UKUMBI WA BASATA: ILALA SHARIFF SHAMBA